Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Thursday, July 19, 2012

Picha ziadi maafa ya meli

Watalii na raia wa kigeni pia walikuwemo katika meli iliyozama hawa ni baadhi ya waliosalimika


Abiria waliookolewa kutoka katika meli iliozama ya Star Gate katika bahari ya Chumbe Zanzibar
Abiria aliyeokoka kutoka katika meli iliyozama
Abiria aliyookoka katika Meli iliozama ya Star Gate akifarijiwa na Jamaa zake Baada ya kuteremka katika Meli iliowaokoa hapo Bandarini(Bofya hapa
HUKu kukiwa bado na tarifa zenye utata juu ya idadi kamili ya waliokufa katika ajali ya meli huko Zanzibar ,mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) imesema, meli iliyozama leo, katika kisiwa cha Chumbe, Zanzibar ilikuwa na abiria 248 wakiwemo watoto 31.
Taarifa ya mamlaka hiyo hiyo imesema, meli hiyo, Mv Skagit iliondoka katika Bandari ya Dar es Salaam leo saa sita mchana, ikiwa na mabaharia tisa.
Kwa mujibu wa Sumatra, meli hiyo, inamilikiwa na Kampuni Seagul Transport, imasajiliwa na Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar (ZMA) na kwamba, Cheti cha Ubora kimeanza tarehe 24 Agosti, 2011 na kinamalizika 23 Agosti, 2012. Imesema, meli hiyo ilikuwa imeruhusiwa kubeba abiria wanaoruhusiwa 300 na tani 26 za mizigo.
“SUMATRA kupitia Kituo cha Utafutaji na Uokoaji (MRCC) ilipata taarifa kuwa meli ya MV Skagit iliyokuwa safarini kutoka Dar es Salaam kuelekea Zanzibar ilikuwa inazama katika eneo la karibu na kisiwa cha Chumbe, Zanzibar, eneo ambalo lipo umbali wa Kilomita za Bahari 13.8 kutoka Bandari ya Zanzibar” imesema taarifa hiyo.
Kwa mujibu wa Sumatra, baada ya kupata taarifa hizo, kituo cha MRCC kilitoa taarifa kwa vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na vyombo vya usafiri wa majini vilivyokuwa karibu na eneo la tukio.
“ Zoezi la uokoaji linaendelea katika eneo la tukio kwa msaada wa vyombo vifuatavyo: Mv Flying Horse, Mv Kilimanjaro III, Tug Bandari ya Zanzibar, KMKM, Mv Zanzibar I, Police Patrol Boat, Navy” imesema taarifa hiyo.

No comments:

Post a Comment