Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Thursday, July 12, 2012

MBOZI WAWAKA KUPAKWA MATOPE

BARAZA la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya wila Mbozi mkoani Mbeya
limekana kuhusika na maamuzi ya kuunda tume ya kuwachunguza baadhi wa
maafisa wa idara ya kilimo wanaotuhumiwa kula fedha za miradi ya
umwagiliaji.

Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Elick Ambakisye amevitupia lawama

baadhi ya vyombo vya habari akisema vinapotosha ukweli wa jambo hilo
na kuzusha mgongano baina ya watendaji na wakazi wa wilaya hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari,Ambakisye alisema hakuna kikao cha

baraza kilichokaa na kuunda tume ya kuwachunguza maafisa kwa tuhuma
zozote kama ilivyoripotiwa.

Alisema kilichopo ni tuhuma za kuchelewa kutumika kwa fedha za baadhi

ya miradi na fedha hizo zinaonekana kuendelea kuwepo katika akaunti za
miradi husika huku miradi ikiwa imesimama.

Alisema umma unapaswa kutambua kuwa uchunguzi unaoendelea ni wa

kuchelewa kutumika kwa fedha na wanaopotosha ukweli huo huenda wana
nia ya kuzorotesha maendeleo ya wilaya hiyo kwa kuchochea migongano.

Aliwasihi wanahabari kufanyakazi kwa kufuata misingi ya kazi zao ili

waendelee kuisaidia jamii kama inavyofanya siku zote.

Hata hivyo mwenyekiti huyo pia aliitupia lawama ofisi ya umwagiliaji

kanada ya nyanda za juu kusini akisema imekuwa kikwazo cha miradi
mingi kutokamilika kwa wakati.

No comments:

Post a Comment