WAJIBU NA HAKI
|
CHAMA CHA WALIMU
TANZANIA (CWT)
(Tanzania Teachers’ Union – TTU)
MKOA WA MBEYA
|
|
P.O. Box
3079 MBEYA
E-mail:
ttumbeyareg@yahoo.com
|
Telephone:
2502535
Cell: 0784-830564
0715-830564
0764-163234
|
Your
Ref: ............................................ Date: 9/7/2012
Our
Ref: CWT/MBY/MW/17/VOL.II/50
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
YAH:
TAARIFA KUWA BAADHI YA WALIMU ‘WAMEIKACHA’ CWT SIYO YA KWELI
Gazeti la
Nipashe la tarehe 9 Julai 2012 ukurasa wa pili iliandikwa taarifa yenye kichwa;
Baadhi ya walimu ‘waikacha’ CWT. Maelezo
haya siyo ya kweli maana walimu hawajajitoa (kuikacha) CWT na wale
walioshawishiwa wajitoe walishindwa maana waliahidiwa na viongozi wa UMET kuwa
mara ukiandika barua ya kujitoa makato yako ya 2% yatasitishwa jambo ambalo
haliwezekani. Kusitishwa kwa makato ni suala la kisheria kuwa Chama kinapofikisha
zaidi ya nusu ya wafanyakazi wa sekta hiyo waliobakia wanatakiwa kukatwa 2% ya
huduma kwa chama (Union Service charge) kwa sheria Na 10 ya Vyama Huru vya wafanyakazi ya 1998
na huduma ya wakala (Agency fee) kwa sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini namba
6 ya 2004. Hakuna sheria inayoruhusu mwanachama kujitoa chama na kufuta makato
na hii ni sheria ya Bunge siyo matakwa ya CWT, maana huwezi kuwa unafaidi
matunda kwa jasho la wenzako (Free rider).
Idadi ya
wanachama wa UMET iliyotajwa kwenye
gazeti la Nipashe hiyo si ya kweli, mfano mkoa wa Mbeya kuwa na wanachama 3,641
si kweli maana wanachama wa CWT Mbeya ni
13,833 kati ya walimu 16,934 hivyo wangekuwa na kiasi hicho (3,641)
Mbeya isingetawalika ki-CWT . Hizo takwimu za wanachamwa UMET wanzipataje
wakati hawajasijiriwa? Je, wanachama wao wanawajuaje? Kw mujibu wa sheria ya
Ajira na Mahusaiano Kazini ya 2004, Ili uwe mwanachama wa chama cha wafanyakazi
chochote lazima uwe umejaza fomu inayoitwa TUF 6 yaani (Trade Union Form Number
6) na baada ya hapo wanachama wanajazwa kwenye daftari la wanachama kwa fomu
namba 15. Je, hao UMET wanachama wao wamewapataje kwama siyo propaganda na
uzushi? Nadhani wanashindwa kutofautisha kati ya wanachama na hisia za kuwa na
washabiki. UMET wanadhani kila anayemshabikia nyoka aliyeuawa anampenda nyoka
kumbe wengine wanataka kuona ukubwa na aina ya nyoka aliyeuawa.Wajaribu
kuchanganua mambo kwa mapana zaid.
Kumekuwa na
taarifa za upotoshaji kwa wanachama na walimu wenye mapenzi mema na CWT yao juu
ya vitega uchumi vya CWT. Kimsingi CWT inakitega uchumi kimoja tu yaani jengo
la ‘Mwalimu House’ lenye ghorofa kumi lililoko
Ilala Boma. Jengo hilo ni la kupangisha na mapatoi yake ni kati y ash, 35 hadi
40 milioni kwa mwezi. Aidha, kuanzishwa kwa kampuni ya walimu TDCL (Teachers’ D
eveolpment Company Limited) wala lengo lake si kufanya biashara bali
ilianzishwa kwa lengo la kupata nafuu ya kodi katika uwekezajiambayo ni sera ya
CWT. Mapato na matumizi ya fedha zote za Chama yanakaguliwa kila mwaka na
mkaguzi wan je fedha toka Kampuni inayotanmbuliwa na kuwasilishwa kwa Msajili
wa vyama vya wafanyakazi. Chama kisipowasilisha ukaguzi wake wa fedha
kinafutwa. Aidha, mwanachama hazuiliwi kuuliza mapato na matumizi ya fedha za
chama kwenye ofisi za CWT hakuna siri
yoyote.
Kwa mantiki
hiyo, maelezo ya UMET ni ya kupotosha walimu na inaonyesha viongoizi wake wanatumiwa
na serikali ili kuwagawa walimu wasidai maslahi bora wakati huu ambapo CWT
kimetangaza mgogoro na serikali. Natoa wito kwa walimu kuwa makini na makundi
haya yanayotumiwa na serikali pamoja na propaganda na vitisho mbalimbali vya
serikali. Wakati ukifika wa mgomo tuungane wote bila woga wala kulinda vyeo
vyetu serikalini kama ualimu mkuu, uratibu, ukuu wa shule, n.k. tudai maslahi
bora kwa walimu wa kizazi hiki ili tuwe tayari kutoa elimu bora kwa watanzania.
Walimu wawe macho na kila namna yoyote ya kuwagawa au kuwachonganisha na CWT
wasahau kuidai serikali maslahi bora. Kila mwalimu anahitaji maslahi bora.
Nawatakia
kazi njema na afya tele.
MSHIKAMANO DAIMA! NA NDIO MKOMBOZI WETU
Mwl. Kasuku Bilago
Katibu CWT Mkoa
Mbeya
No comments:
Post a Comment