NIGERIA U20 YAWASILI KUIKABILI NGORONGORO HEROES
Flying
Eagles itapambana na Ngorongoro Heroes katika mechi ya kwanza ya
raundi ya pili itakayofanyika Jumapili (Julai 29 mwaka huu) kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.
Mechi
hiyo ya kuwania tiketi ya kucheza fainali za 18 za Afrika kwa vijana
wenye umri chini ya miaka 20 zitakazochezwa mwakani nchini Algeria
itachezeshwa na waamuzi kutoka Kenya wakati Kamishna ni Charles Masembe
kutoka Uganda.
Flying
Eagles inayofundishwa na kocha John Obuh, jana (Julai 24 mwaka huu)
ilicheza mechi ya kirafiki na Rwanda (Young Amavubi) kwenye Uwanja wa
Amahoro jijini Kigali. Nigeria ililala bao 1-0.
Msafara
wa timu hiyo unaongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Nigeria (NFF), Chris Green. Baadhi ya
wachezaji walioko katika kikosi cha Flying Eagles ni Chidi Osuchukwu,
Alhaji Gero, Shehu Abdullahi, Aminu Umar, Aliyu Mohamed, Uche Agbo,
Jonah Usman, Harrison Egbune, Hassan Abubakar na Yahya Adamu.
Viingilio
katika mechi hiyo vitakuwa sh. 3,000 kwa viti vya rangi ya chungwa,
bluu na kijani wakati VIP B na C itakuwa sh. 5,000. Kiingilio kwa VIP A
itakuwa sh. 10,000.
NUSU FAINALI KOMBE LA KAGAME
Nusu
fainali zote mbili za kuwania Klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati
(Kombe la Kagame) mwaka 2012 zinachezwa kesho Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 15,000 na sh. 20,000.
Azam
na AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) zitacheza nusu
fainali ya kwanza kuanzia saa 8 kamili mchana, na kufuatiwa na nusu
fainali ya pili kati ya Yanga na APR ya Rwanda itakayoanza saa 10 kamili
jioni.
MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kesho litakuwa na mkutano na
waandishi wa habari. Mkutano huo utafanyika ofisi za TFF saa 5 kamili
asubuhi.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment