MATREKTA madogo(Powertiller) 40 yaliyonunuliwa na
halmasahauri ya wilaya ya Chunya na kusambazwa vijijini hayafanyi kazi.
Kwa mujibu wa mkuu wa wilaya hiyo Deodatus Kinawiro
matrekta hayo yaliyoigarimu serikali zaidi ya shilingi milioni 217 hayajafanya
kazi yoyote tangu yapelekwe vijijini ikiwa ni zaidi ya mwaka sasa umepita huku
sababu za kutotumika zikiwa hazifahamiki.
Kinawiro aliyasema hayo katika kikao maalumu cha
baraza la madiwani kilicholenga kujadili taarifa ya mdhibiti na mkaguzi wa
hesabu za serikali(CAG) kilichokuwakikiongozwa na mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas
Kandoro.
Aliyasema hayo kufuatia mkuu wa mkoa kuhoji iwapo
matrekta yanayotajwa katika moja ya hoja za CAG kwenye taarifa yake ya mwaka wa
fedha 2010/2011 kuwa mpaka ukaguzi unafanyika matrekta hayakuonekana licha ya
fedha kutumika na ndipo madiwani wakajibu kuwa yalinunuliwa na kusambazwa
vijijini.
Hata hivyo mkuu wa wilaya aliwashangaa madiwani haoa
kisema hawasemi ukweli juu ya matumizi ya matrekta hayo kwani hayafanyi
shughuli iliyolengwa na serikali ya kuwapunguzia wakulima adha ya kulima kwa
mkono.
Kinawiro alitolea mfano katika kata ya Ifumbo kuliko
na mradi mkubwa waumwagiliaji akisema zilipelekwa Powertiller nne na tatu kati
ya hizo zimeendelea kukaa bila matumizi na moja inatumiwa kwa shughuli za
kubeba mchanga na mawe na si kulimia.
Alisema kama serikali ya wilaya tayari wamemuandikia
barua mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ili aeleze ni kwa nini powertiller
hizo hazijaanza kuwasaidia wakulima kama maelekezo ya serikali yanavyoeleza.
Alisema pia serikali kuu imepeleka fedha kwaajili
yakununua powertiller nyingine kumi lakini amezuia ununuzi huokwakuwa 40 za
kwanza hazijaonekana kufanya chochote.
“Tunalazimika kuhoji zile za awali hazifanyi kazi
mpaka sasa kuna haja gani ya kununua nyingine 10.Tumeiuliza halmashauri na sasa
tunasubiri majibu kutoka kwa mkurugenzi” alisema.
No comments:
Post a Comment