MWINGILIANO wa masafa ya televisheni uliotokea hivi
karibuni katika baadhi ya maeneo ya Jiji la Mbeya umeelezwa kusababishwa na
masafa yaliyokuwa yakitumika kuchukuliwa na wamiliki wake halali walioyanunua.
Hayo yamebainishwa leo na Meneja wa mamlaka ya mawazsiliano
nchini(TCRA) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Deogratius Moyo alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.
Moyo amesema kuwa masafa hayo hivi sasa yanatumika kutolea huduma za
Interneti kwa makampuni yanayotoa huduma hiyo nchini.
Amesema kwa watumiaji wa dishi ya Setilaiti wanatakiwa kufanya
marekebisho ya madishi yao ili waweze kupata masafa sahihi yanayorusha
matangazo kwenye masafa yaliyotengwa kwa ajili ya matangazo ya Televisheni.
Akifafanua zaidi, Meneja huyo amesema masafa ya
sataelaiti katika C-Band huanzia 3.7GHZ hadi 4.2GHZ yametengwa kwa ajili ya
intaneti barani Afrika huku masafa hayo katika C- Band huanzia 3.4GHZ hadi
3.6GHZ ni kwa ajili ya ukanda wa Afrika Mashariki.
Akizungumzia tatizo la masafa katika jiji la Mbeya,
Moyo amesema kuwa kwa kuwa wananchi wengi walifunga kifaa cha kunasa mawimbi
(NLB) kwenye uelekeo wa masafa ya intaneti ambayo wamiliki wake walikuwa
hawajaanza kuyatumia, na kuwa baada ya wamiliki halali kuyachukua imesabaisha
baadhi ya watu kukosa matangazo ya televisheni.
Meneja huyo amesema masafa hayo kwa hivi sasa
yanatumiwa na kampuni ya simu ya Vodacom, hivyo watumiaji wengine hawana budi
kuhama na kubadilisha kifaa cha kunasa matangazo kwa njia ya sataelaiti (LNB).
Amesisitiza wananchi kujiunga na mfumo wa digitali
kwa kuwa ifikapo Desemba 31, mwaka huu mitambo ya kurushia matangazo kwa njia
ya analojia itazimwa nchini huku akiusifia mfumo mpaya akisema ni salama, hauna
madhara wala gharama kubwa kwa mtumiaji.
No comments:
Post a Comment