Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Saturday, January 25, 2014

AFISA UGANI APEWA MWEZI MMOJA KUCHAGUA KUACHA KAZI AU KUFUATA MASHARTI YA KAZI YAKE

Mkuu wa mkoa wa Mbeya akimnyooshea kidole kama ishara ya kumuonya afisa ugani wa kata ya Myovizi wilayani Mbozi Rehema Mwandurusa kwa kugoma kuishi kituoni kwake Afisa ugani wa kata ya Myovizi wilayani Mbozi Rehema Mwandurusa mwenye gauni lenye madoa meusi na meupe akisikiliza maagizo toka kwa mkuu wa mkoa huku akiwa anarekodi kwa simu yake ya kiganjani. OFISA ugani wa kata ya Myovizi wilayani Mbozi Rehema Mwandurusa amepewa muda wa mwezi mmmoja kuhamika eneo lake la kazi ama sivyo atakuwa amepoteza ajira yake. Agizo hilo lilitolewa na mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro alipokuwa katika mkutano na wakazi wa kata hiyo uliofanyika kijijini Ichesa juzi. Agizo hilo lilitokana na wakazi wa kata hiyo kubainisha kuwa afisa huyoamekuwa akishindwa kuwajibika ipasavyo katika majukumu yake kutokana na kuishi mbali na kituo chake cha kazi. Walisema wamekuwa wakiishi kama hawana mtaalamu wa kilimo hivyo kulazimika kuendesha shughuli zao pasipo utaalamu wowote jambo walilosema linawakwamisha kupia hatua za kimaendeleo kupitia kilimo. Mwenyekiti wa halmashauri wa wilaya ya Mbozi Eliki Ambakisye pia alikiri afisa huyo kukaidi agizo la kumtaka aishi eneo lake la kazi na badala yake amekuwa akiishi katika mji mdogo wa Mlowo uliopo takribani kilomita kumi kutoka eneo hilo. Ambakisye pia alisema kwa kuishi mbali na eneo la kazi afisa huyo amekuwa akifika kwa kusua sua sana katika eneo hilo hivyo uwepo wake hauwasaidii wananchi aliopewa dhamana ya kuwatumikia. Kufuatia malalamiko hayo,Kandoro alimuagiza afisa huyo kuchagua jambo moja kati ya kazi na kuishi anakotaka yeye ili nafasi yake apewe mtu aliye na utayari wa kuishi katika eneo lake la kazi ili kuwatumikia wananchi “Binti nakupa mwezi mmoja kufanya maamuzi.Unataka kazi hamia hapa,hautaki endelea kuishi unakotaka.Ndani ya mwezi mmoja usipokuwa umehamia hapa jua kabisa ajira yako haipo tena.Naomba mkurugenzi ufuatilie jambo hili na unipe taarifa”

No comments:

Post a Comment