Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Friday, January 10, 2014

HOSPITALI YA MAKANDANA YAEZULIWA KWA KIMBUNGA

HOSPITALI ya Makandana wilayani Rungwe ni miongoni mwa majengio laliyoathiriwa na kimbunga kikubwa kilichotokea juzi katika mji mdogo wa Tukuyu na kusababisha hasara ya kuharibika kwa mali. Kimbunga hicho cha upepo mkali kilichoambatana na mvua kilitokea juzi majira ya saa sita mchana na kudumu kwa muda wa dakika kumi huku kikiacha hasara ya kuezua na kubomoa majengo mbalimbali pamoja na kuangusha miti. Akizungumza na Lyamba Lya Mfipa ofisini kwake,mganga mkuu wa gospitali ya Makandana Stanfod Mwakatage alilitaja jengo la wagonjwa wa nje kuezuliwa paa na kusababisha maji ya mvua kulowanisha vifaa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi. Dk.Mwakatage alisema katika vifaa vilivyolowa maji ni pamoja na mashine mbalimbali zenye gharama kubwa ambazo haijafahamika iwapo zimeharibika au la kwani ilikuwa vigumu kuziwasha kwa hofu ya kuziharibu zaidi iwapo maji yaliingia kwa ndani. “Ni vigumu kujua iwapo vimeharibika kwani tunaogopa kuviunganisha katika umeme vinaweza kuharibika iwapo maji yaliingia kwa ndani.Tunasubiri upite muda wa kutosha ndipo tuanze kujaribu na hapo tutaweza kujua iwapo mashine hizi zimeharibika” “Ni mashine za mamilioni kwakweli itakuwa hasara kubwa iwapo zitakuwa zimeharibika kwa kuingiza maji.Lakini uhakika tutaupata tukizijaribu” Alisemaa pia majui yaliyoingia kupitia paa lililoezuliwa pia yaliweza kuathiri chumba cha kumbukumbu kwa kulowanisha majalada kati ya 100 na 150 yaliyokuwa ndani ya chumba hicho. Alisema ni muhimu chumba hicho kikaezekwa haraka kutokana na umuhimu wake hospitalini hapo na kubainisha kuwa jitihada mbalimbali zimekwisha anza kuchukuliwa ili kukirejesha katika hali yake ya kawaida.

No comments:

Post a Comment