Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Sunday, January 12, 2014

MADEREVA WA BODA BODA MBEYA KUANDALIWA LIGI YA SOKA

Mkurugenzi wa matukio na Uratibu wa kampuni ya Citysign Promotion & Marketing Agency Limited ya jijini Mbeya Geofray Mangungulu akifafanua jambo katika kikao cha kwanza cha maandalizi ya mashindano ya soka kwa madereva wa boda boda kilichofanyika Mbeya New City Pub KAMPUNI ya Citysign Promotion & Marketing Agency Limited ya jijini Mbeya inataraji kuandaa mashindano ya mpira wa kwa timu za madereva wa boda boda jijini Mbeya. Bodi ya wakurugenzi wa kampuni hiyo,jana ilikaa na viongozi wa Umoja wa waendesha boda boda jijini hapa(UWABOM) katika kikao cha kwanza na kujadili kwa pamoja namna mashindano hayo yanapaswa kuendeshwa. Akizungumza katika kikao hicho Mkurugenzi wa matukio na Uratibu Geofray Mangungulu alisema mashindano hayo yatafanyika april mwaka huu na kujumuisha timu mbalimbali kutoka kanda sita za UWABOM. Mangungulu alisema lengo la mashindano hayo ni kudumisha amani na mshikamano baina ya waendesha boda boda na pia kuondoa imani potofu dhidi yao iliyejengeka katika jamii kuwa madereva hao ni wakorofi na wasio na ushirikiano mzuri na jamii. “Watu wwengi wanaamini kuwa madereva wa boda boda ni wakorofi na hata wao wenyewe hawaelewani.Tunaamini kupitia mashindano ya kimichezo madereva hawa wanaweza kuionyesha jamii inayowazunguka kuwa wao ni wamoja na hawana tofauti yoyote na jamii nyingine” alisema Mangungulu. Alisema pia kupitia mashindano hayo madereva hao watanufaika sit u kwa mabingwa kukabidhiwa kombe na zawadi,bali pia kwa pamoja washiriki wote wataweza kupewa elimu juu ya ujasiriamali,umuhimu wa kujiunga na bima ya afya na pia kujiwekea akiba benki. Alisema taasisi mbalimbali wadau wanatarajiwa kupewa mualiko wakati mashindano yatakapokuwa yanaendelea amabpo watafika na kuweza kutoa elimu juu ya guduma wanazotoa na kutoa ufafanuzi ni kwa namna gani madereva wa boda boda wanaweza kujiunga na kunufaika nazo. “Kupitia mashindano haya madereva wa boda boda pia watapewa elimu ya namna na jinsi gani wanaweza kunufaika iwapo wataanzisha chama cha kuweka na kukopa yaani Saccos yao.Lakini pia wahamasishwe kuhusu suala la usalama kwanza” alifafanua. Kwa upande wao mwenyekiti wa UWABOM Vincent Mwashoma na katibu wake Msumba Mbesa waliipongeza kampuni hiyo kwa kuwaletea wazo walilosema lina manufaa makubwa katika jamii ya waendesha boda boda. Hata hivyo mwenyekiti wa kamati ya ufundi wa chama cha soka Mbeya mjini(MUFA) Ramadhan Luwandala alisisitiza suala la nidhamu kimechezo kuanza kusisitizwa katika vikao vyote vya maandalizi ya mashindano hayo akisema tayari jamii ya waendesha boda boda ilikwisga onesha sura ya vurugu katika mashindano mbalimbali.

No comments:

Post a Comment