Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Wednesday, January 15, 2014

HOSSANA OWS CENTRE YAWANOA WANA KAMATI ZA AFYA ZA KATA TAYARI KWA UTEKELEZAJI WA MRADI WA UWAJIBIKAJI KATIKA MIRADI YA AFYA ILEJE

Mmoja wa wawezeshaji katika semina iliyoambatana na uundwaji wa kamati za kufuatilia mradi wa Kuimarisha Uwajibikaji wa jamii ya Ileje katika kusimamia mipango ya maendeleo ya sekta ya afya katika ngazi ya Kijiji,kata na wilaya unaoendeshwa na shirika la Hossana OWS Centre Bw.John Ngogo akiendelea kufundisha darasa lililohudhuliwa na washiriki kutoka kata tatu za Itumba,Isongole na Mlale.Mradi huo unaendeshwa katika kata 16 za wilaya ya Ileje kwa ufadhili wa The Foundation For Civil Society. Washiriki wakifuatilia kwa makini maelezo ya mradi na mikakati inayowapasa kwenda kuitekeleza baada ya kuunda kamati za afya za kata Hapa wakimsikiliza mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Hossana OWS Centre Bw.Nsanya Mwalyego aliyewabainishia lengo la mradi huo wenye manufaa makubwa kwa jamii ya wana Ileje. ,Washiriki wakiwa katika makundi yaliyogawanyika kwa kila kata tayari kwa kuunda kamati za Afya za kata zitakazokuwa na majukumu mbalimbali ikiwemo kufuatiolia miradi ya afya kwenye kata zao pamoja na kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa Uwajibikaji katika miradi ya afya iliyopo kwenye vijiji na kata zao.Mradi huu ni wa miaka mitatu.

No comments:

Post a Comment