Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Friday, January 10, 2014

RUNGWE KUKUSANYA BILIONI 50

JUMLA ya shilingi 50,984,381,888 zinatarajiwa kukusanywa na halmashauri ya wilayaa ya Rungwe mkoani Mbeya katika kipindi cha mwaka wa fedha 2014/2015. Katika mwaka wa fedha 2013/2014 unaoendelea hivi sasa halmashauri hiyo ilijiwekea matarajio ya kukusanya shilingi 48,669,115,528. Hayo yalibainishwa na Afisa Mipango wa halmashauri hiyo Elias Sangi alipokuwa akiwasilisha mapendekezo ya bajeti ya mwaka huo wa fedha kwenye kikao cha balaza la madiwani kilichofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri hiyo. Sangi alisema kati ya fedha hizo,mapato kutoka vyanzo vya ndani yatakuwa shilingi 2,086,077,300, ruzuku ya mishahara ya wafanyakazi kutoka serikali kuu ni shilingi 26,577,225,607. Mapato kwaajili ya matumizi mengineyo itakuwa shilingi 2,801,999,823,miradi ya maendeleo na mifuko ya pamoja ni shilingi 6,873,610,496 wakati maombi ya fedha kwaajili ya ya miradi ya kitaifa ya maji na umwagiliaji ni shilingi 12,645,468,662. Hata hivyo Sangi alizitaja changamoto zinazoikabili halmashauri katika utekelezaji wa mikakati na bajeti zake kuwa ni pamoja na upungufu wa wataalamu hususani katika sekta za afya,elimu,ardhi na maji hali inayochangia kuzorotesha kwa kiasi kikubwa hali ya utoaji huduma bora kwa wananchi. “Upungufu wa vitendea kazi hususani magari na vifaa vingine vya ofisi kutokana na kugawanywa kwa halmashauri ya Rungwe na kuunda halmashauri mbili za Rungwe na Busokelo” alisema Sangi na kuongeza. “Uhaba wa nyumba za watumishi hususani walimu katika shule za msingi na sekondari na watoa huduma za afya ya msingi hivyo kusababisha watumishi hao kufanya kazi katika mazingira magumu.” Afisa mipango huyo aliitaja pia changamoto ya viwango vidogo vya ukomo wa bajeti ambavyo havijaongezwa toka mwaka wa fedha 2009/2010 na hivyo kusababisha halmashauri kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo kwa kuzingatia gharama za uendeshaji zinapanda mara kwa mara.

No comments:

Post a Comment