Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Monday, January 13, 2014

WAWILI WAUAWA KIKATILI MBEYA

JINAMIZI la watu kujichukulia sheria mikononi na kukatika uhai wa wenzao limezidi kushika kasi mkoani Mbeya baada ya watu wawili kuuawa juzi(Januari 12) katika matukio mawili tofauti. Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Ahmed Msangi alisema tukio la kwanza lilitokea katika kijiji cha Lema kata ya Ngana wilayani Kyela majira ya saa 11:00 alfajiri. Kamanda Msangi alisema katika tukio hilo mkazi wa mkazi wa kijiji hicho Bicco Mwakibibi(28) aliuawa kwa kupigwa sehemu mbalimbali za mwili wake na kundi la wananchi walioamu kujichukulia sheria mikononi wakitumia silaha za jadi ikiwemo mawe na fimbo. Alisema wananchi wao walikuwa wakiwatuhumu Biko na mwenzake amabye hakufahamika jina lake kwakuwa alikimbia kuwa walivunja kibanda kimoja cha biashara kijijini hapo na kuiba. Kamanda huyo alisema mauaji mengine yalitokea katika kijiji cha Kapele wilayani Momba ambapo mkazi wa kijiji hicho Adam Silumbe(27) alifariki dunia alipokuwa akipata matibabu katika hospitali ya wilaya ya Mbozi kufuatia majeraha ya kuchomwa kisu mgongoni na mdogo wake aliyemtaja kwa jina la Bonny Silumbe. Alisema chanzo cha mauaji hayo ni kulipiza kisasi kwakuwa marehemu alimtangaza mdogo wake kijijini kwao kuwa alimtorosha mke wa mtu hatua iliyomkasirisha mdogo wake. Alisema mtuhumiwa alikimbia mara baada ya tykio na anaendelea kutafutwa wakati mwili wa marehemu ukiwa umefanyiwa uchunguzi na kukabidhiwa kwa ndugu kwaajili ya maziko. Kamanda Msangi alitoa wito kwa jamii kuacha kujichukulia sheria mkononi na badala yake wafuate njia sahihi za kuwafikisha watuhumiwa katika mamlaka za kisheria zilizopo japo ni kauli ambayo kila kukicha imekuwa ikitolewa na inaonekana kutokuwa na nguvu katika jamii ya wakazi mkoani hapa.

No comments:

Post a Comment