Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Monday, January 20, 2014

MAHAFALI YA WANACHAMPION MBEYA YAFANA

JAMII ya wanandoa imesisitizwa kufanya mazungumzo ya pamoja na kumaliza mafarakano kwa haraka pale inapobainika mmoja kwenda kinyume na utaratibu ndani ya nyumba zao. Imeelezwa kuwa kwa kufanya hivyo jamii hiyo itaweza kuishi kwa furaha na upendo zaidi kuliko ilivyo kwa wanandoa wanaoamua kukaa kimya pale wanapokosewa na kubaki wakiumizwa na jambo husika moyoni. Hayo yalibainishwa na mmoja wa watu wanaoishi na virusi vya ukimwi(VVU) jijini Mbeya Ester Kipapa alipokuwa akitoa ushuhuda wa kuishi na virusi hivyo kwenye mahafali ya kuhitimu mafunzo ya miezi mitatu ya kupunguza maambukizi ya VVU kwa wanaume kuwajibika yalioandaliwa na shirika la Engenda Health kupitia mradi wake wa Champion. Kipapa alisema kwa wanandoa kuvunja ukimya na kuzungumza itawezesha kuwa na mipango ya pamoja ikiwa ni pamoja na kupima afya zao na kuzijia hali itakayowezesha pia wanandoa hao kuzaa watoto bila maambukizi ya VVU kwakuwa watakuwa wanazifahamu afya zao tayari. “Nawasihi vijana wangu hakikisheni mnavunja ukimya.Zungumzeni na wenzi wenu mkapime ili maze watoto wasio na maambukizi.Nashukuru pia kwa elimu tuliyoipata kupitia mafunzo haya kwani yamezidi kuniongezea ujasiri wa kuendelea kutoa elimu kwa wanangu na jamii yote inayonizunguka” alisema. Mhitimu mwingine wa mafunzo hayo Sekela Mpoli alisema elimu waliyoipata imemwezesha kuishi pasipo kuwanyanyapaa watu waishio na VVU na Ukimwi tofauti na awali alipokuwa akiogopa kushirikiana nao katika shughuli au maongezi mbalimbali huku pioa akisema amepata uwezo wa kutoa elimu kuwabadilisha wanaume wanaowatendea ukatili wenzi wao. Akisoma risala ya wahitimu,mmoja wa wahitimu Geofray Kindimba,alisema mafunzo hayo yalianza Oktoba 14 mwaka jana yakiwa na washiriki 240 lakini baadaye walipungua na kubaki 216. Akifunga mafunzo hayo kwa niaba ya mganga mkuu wa mkoa wa Mbeya Seif Mhina,mratibu wa huduma za chanjo mkoani hapa Japhet Mhai aliwataka wahitimu kutambua kuwa vyeti walivyopewa ni heshima na zawadi kwao lakini wasipowajibika kwa kuwa mabalozi wazuri watakuwa hawavitendei haki.

No comments:

Post a Comment