Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Sunday, January 5, 2014

ZIARA YA UKAGUZI MADUKA NA MAGHALA YA MBOLEA ILIVYOBAINI MAPUNGUFU MENGI

Ziara ya maafisa udhibiti wa mbolea mkoa wa Mbeya ilianzia katika mji mdogo wa Mbalizi wilayani Mbeya.Hapa yalibainika mapungufu kama kuhifadhi mbolea juani kama inavyoonekana hapa ambapo muuzaji ambaye hakufahamika jina alijificha baada ya kuwaona maafisa hawa Katika duka hili la Kalinga jambo la kwanza mbolea ilikutwa juani.Lakini pia mmiliki wa duka hili hajajisajiri kama muuzaji mbolea kama inavyoelekezwa na Mamlaka ya udhibiti wa mbolea Mmiliki wa duka hili Bw.Kalinga yeye hakuwakimbia maofisa hawa,alikutana nao na kujieleza ni kwa nini anakiuka maelekezo ya uhifadhi na uuzaji wa mbolea. Shughuli pevu ni katika ghala la kampuni ya Yara eneo la Iwambi jijini Mbeya.Hapa maafisa hawa walikuta shehena kubwa ya mbolea ikiwa imewekwa sakafuni jambo ambalo husababisha mbolea kupoteza ubora wake kwani inakuwa ikinyonya unyevu toka sakafuni Safari ikaendelea hadi katika ghala la kampuni ya Premium inayomilikiwa na wafanyabiashara wenye asili ya Kiasia.Hapa maafisa wakabaini sehemu ya jengo la ghala kuvuja maji mvua inaponyesha hali inayohatarisha ubora wa mbolea iliyohifadhiwa kabla ya kumfikia mkulima Sasa ni kuelekea Mwanjelwa,Sido,Mama John na kisha uyole Kwa uyole maduka yote wauzaji walikuwa wameianika mbolea juani huku maghala yao pia mifuko ya mbolea ikiwa imepangwa bila kufuata utaratibu wa kuacha sentimita za kutosha upande wa ukutanani.Pia magjala hayana hewa wala mwanga wa kutosha Na huu ukawa mwisho wa ziara yetu.Aksanteni kwa kuwa nasi.Endelea kutembelea Lyamba Lya Mfipa.

No comments:

Post a Comment