Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Wednesday, January 15, 2014

MTOTO HUYU AMETELEKEZWA TANGU DESEMBA 23 MWAKA 2013

Mtoto huyu aliyepewa jina la Baraka kutokana na jina lake la awali kutofahamika ameendelea kulelewa na msamaria mwema anayejishughulisha na biashara ya mama lishe katika moja ya vibanda vilivyopo eneo la Standi kuu ya jijini Mbeya. Msamaria huyo aliyejitambulisha kwa jina la Subira Mwaijulu aliiambia Lyamba Lya Mfipa kuwa mtoto huyo anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya mwaka mmoja na nusu hadi miwili alitelekezwa nje ya kibanda chake akiwa ananyeshewa na mvua kubwa mnamo Desemba 23 mwaka jana na mtu asiyefahamika na mpaka sasa haijulikani wazazi wa mtoto huyo wanapatikana wapi.Kwa yeyote anayewafahamu wazazi wa mtoto huyu anaweza kuwasiliana na mhariri mkuu wa Lyamba Lya Mfipa kupitia 0756 40 95 97 au kufika katika kibanda cha Sunche Mama lishe kilichopo Stendi kuu.Tushirikiane kupata ufumbuzi wa tatizo hili.Mungu akubariki

No comments:

Post a Comment