Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Friday, January 17, 2014

HATARIIII,CHOO HIKI KINATUMIWA NA WAKAZI WA KATA YA ILEMBO

WAKAZI wa kata ya Ilembo wilayani Mbeya na maeneo ya jirani wanakabiliwa na hatari kukumbwa na magonjwa ya mlipuko kufuatia kukosekana kwa vyoo bora katika eneo linalotumiwa kwaajili ya soko la ijumaa. Hali hiyo imebainika jana,wakati Lyamba Lya Mfipa ilipofika katika soko hilo lililopo katika eneo la madukani na kujionea ukosefu wa vyoo bora ulivyo changamoto kwa watu wanaofanya shughuli sokoni hapo na wateja wao. Eneo hilo lilionekana kuwa hatari zaidi kufuatia uwepo wa vilabu vya pombe za kienyeji kwa wingi hali inayosababisha kuwepo kwa msongamano mkubwa wa watu ambao afya zao ziko hatarini. Kwa upande wa wanywaji wa pombe za kienyeji katika vilabu hivyo wamekuwa wakilazimika vyoo vilivyojengwa choo kimoja kilichojengwa kienyeji kikiwa ni kichafu na kisichostahili kutumiwa na binadamu. Kufuatia hali hiyo baadhi ya watu wamekuwa wakilazimika kujisaidia katika mapagala,vichaka na hata upenuni mwa majengo yaliyopo jirani hususani nyakati za usiku. Akizungumzia changamoto hiyo,Diwani wa kata ya Ilembo Patrick Mwasenga amekiri afya za wakazi kuwa hatarini lakini akasema jitihada mbalimbali zinafanyika ili kupata ufumbuzi ikiwa ni pamoja na kuwahimiza wamiliki wa majengo waliyopaangishwa wafanyabiashara wa vilabu kujenga vyoo bora. Lakini afisa mtendaji wa kata ya Ilembo Jailo Shila mesema tayari uongozi wa kata ulitoa maagizo ya wamiliki hao kujenga vyoo bora haraka iwezekanavyo na kati yao ni mmoja tu aliyekwisha chimba shimo nab ado hajaanza kujenga hadi sasa.

No comments:

Post a Comment