Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Saturday, January 4, 2014

ASKARI WAWILI MBARONI KWA UJAMBAZI

WATU watano wakiwemo askari wawili wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Mbeya kwa tuhuma za kuwaka na kisha kuwapora mali mbalimbali ikiwemo fedha taslimu wafanyabiashara wenye asili ya kiasia. Askari wanaoshikiliwa ni wa jeshi la polisi wa kazi za kawaida wilayani Mbeya F 8302 PC James(32) na askari magereza wa gereza la Ruanda lililopo jijini Mbeya B 500 SGT Juma Musa(38). Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Kamishina msaidizi mwandamizi Ahmed Msangi amewataja wengine waliokamatwa kuwa ni wakazi wa Forest jijini Mbeya Mbaruku Hamis(29),Amri Kihenya na Elinanzi Mshana(29) aliyesema ni mzoefu katika wizi na ujambazi. Kamanda Msangi amesema watuhumiwa hao wamefanya uporaji huo Januari 3 saa 11:35 katika eneo la Mlima Kawetere barabara ya Mbeya/Chunya baada ya kumteka mfanyabiashara mwenye asili ya kihindi Sreedhar Pasupeleti(38) mkazi wa Makata wilayani Chunya akiwa safarini na wenzake wawili wakitokea Mbeya kwenda Chunya. Amesema jambazi hao waliokuwa na pingu na panga moja baada ya kuwateka wafanyabiashara hao waliwapora fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni tatu,mabegi matatu yaliyokuwa na nguo,Kompyuta mpakato moja aina ya Sumsang,simu ya kiganjani aina ya Sumsang pia na mablanketi mawili.

No comments:

Post a Comment