Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Tuesday, January 21, 2014

ZIARA YA KIKAZI YA RC KANDORO WILAYANI MBOZI

. Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akizungumza na viongozi mbalimbali wa wilaya ya Mbozi baada ya kukagua ghala la mazao lililopo katika kata ya Harungu wilayani hapo alipokuwa kwenye ziara ya kikazi.Ghala hillo ni miongoni mwa maghala 54 yatakayofanyiwa ukarabati wilayani hapa kwaajili ya utekelezaji wa mpango wa Matokeo Makubwa sasa kupitia mpango wa Stakabadhi ghalani. Mjumbe wa bodi ya chama cha msingi cha ushirika cha Hampangui Andrea Nyingi akisoma taarifa ya Ghala hilo lililojengwa mwaka 1983 lakini miaka sita iliyopita liliacha kutumika kutokana na kufa kwa vyama vya ushirika. Mkuu wa mkoa akiangalia mizinga ya nyuki inayotengenezwa na Diwani wa kata ya Harungu Samson Simkoko anayetaka kujikita katika ufugaji huo unaosisitizwa na serikali.Diwani huyo alipata hamasa ya ufugaji nyuki baada ya kwenda ziara ya mafunzo mjini Dodoma katika shamba la nyuki la waziri mkuu.Watu mbalimbali pia wamekuwa wakifika kwa diwani huyu kujifunza namna ya utengenezaji wa mizinga ya kisasa Diwani wa kata ya Harungu Samson Simkoko akielezea manufaa watakayoyapata wakazi wea kata yake pale serikali itakapofanya ukarabati wa ghala lililopo kwenuye kata hiyo Mhariri mkuu wa Lyamba Lya Mfipa akipiga stori na watoto wakazi wa kijiji cha Harungu waliogoma kata kata kutaja majina yao Safari ya Mkuu wa mkoa ikaendelea mpaka katika katika kata ya Isansa zilipo ofisi za Iganda Coffee Group.akiwa hapa akajionea changamoto mbalimbali zinazokikabili kikundi hiki cha wakulima wadogo wa kahawa ikiwa ni pamoja na udogo wa mashine isiyokidhi wingi wa kahawa inayopaswa kukobolewa.Hapo aliahidi serikali kuona uwezekano wa kukiwezesha kikundi kupanda mashine kubwa ili wasije wakarudi katika zama za kuuza kahawa mbichi kwa makampuni makubwa hali inayoweza kuwapa hasara.Msimamo wa serikali mkoani hapa ni mkulima kukoboa kahawa yake na kuiuza ikiwa imekaushwa. Mazao yaliyoonekana kustawi katika mashamba yalionekana kumvutia kwa kiasi kikubwa mkuu huyu wa mkoa.Hakusita kuwamwagia sifa wakazi wa kata hii na kuwasihi kuendelea kujituma katika ajira ya kilimo na kuahidi serikali itazidi kuwasaidia katika kutafuta soko la uhakika. . Baada ya kupokea taarifa ya kikundi hiki,Kandoro na wajumbe wengine wa msafara wakaambatana na wenyeji wao kutembelea bwawa lililochimbwa maalumu kwaajili ya kuhifadhia maji ya kukobolea kahawa.Lakini huku akaonekana kutopendezwa na bwawa hilo.Ni kutokana na kuona kuwa lina uwezo wa kuhifadhi maji kidogo yasiyotosheleza mahitaji,halina kingo pembezoni na pia mifugo hasa ng'ombe wanalishwa kiholela hadi lilipo bwawa hilo.Akaagiza kuhakikisha mhandisi wa halmashauri ya Mbozi anafika na kuangalia uwezekano wa kuliongezea kingo ndefu ili liweze kuhifadhi maji mengi na pia akatoa myda wa miezi miwili kwa kikundi husika kupanda miti na katani kuzunguka bwawa hilo. .ZIARA IKAISHIA HAPO NA SASA WENYEJI WANAWASINDIKIZA WAGENI TAYARI KWA SAFARI YA KURUDI JIJINI MBEYA NA KUWAACHA WAKAZI WA ISANSA WAKIWA NA MATUMAINI KWA KUFIKIWA NA KIONGOZI WAO.

No comments:

Post a Comment