Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Sunday, January 19, 2014

MAANDALIZI BODA BODA CUP 2014 YASHIKA KASI MBEYA

Mkurugenzi wa matukio na Uratibu wa kampuni ya Citysign Promotion & Marketing Agency Limited ya jijini Mbeya Geofray Mangungulu akifafanua jambo katika kikao cha pili cha maandalizi ya Boda boda Cup 2014 kilichofanyika jana pale New Mbeya City Pub. AFISA KUTOKA MFUKO WA PENSENI WA PPF NYEMO CHOMOLA AKITOA UFAFANUZI WA UMUHIMU WA WAENDESHA BODA BODA KUJIUNGA NA MFUKO HUO KWA MANUFAA YAO YA BAADAYE ,WAANDISHI WA HABARI EMANUEL LENGWA WA ITV/NIPASHE(KUSHOTO) NA HOSEA CHEYO WA TBC WAKIFUATILIA KWA MAKINI HOJA KATIKA KIKAO HICHO ,mwenyekiti wa kamati ya ufundi wa chama cha soka Mbeya mjini(MUFA) Ramadhan Luwandala akisisitiza suala la nidhamu kwa madereva wa boda boda waatakaoshiriki michuano hiyo Maandalizi ya mashindano ya soka ya waendesha bodaboda(Boda Boda Cup 2014) yamezidi kushika kasi baada ya kufanyika kwa kikao cha pili cha maandalizi hayo kilichowakutanisha maafisa wa kampuni ya Citysign Promotion & Marketing Agency Limited ya jijini Mbeya na viongozi wa vituo mbalimbali vya waendesha boda boda. Kupitia kikao hicho cha pili pande hizo mbili zimekubaliana kwa pamoja kanda jumla ya timu 16 zitashiriki michuano hiyo ambapo kanda kubwa nne zitatoa timu tatu kila moja na kanda mbili zilizo ndogo zitatoa timu mbili mbili kila moja.

No comments:

Post a Comment