Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Thursday, June 14, 2012

WANAUME wanaofanyiwa unyanyasaji na wake zao ikiwemo kupigwa  wamehimizwa kujiunga katika chama chao ili kiweze kuwasaidia kupigania haki zao zilizo za nmsingi.
Afisa kutoka kituo cha usimamizi wa sheria na haki za binadamu(LHRC) Reticia Petro alitoa hamasa hiyo katika semina ya siku tatu ya mafunzo juu ya usimamizi wa sheriaa na haki za binadamu iliyofanyika jijini Mbeya na kuhudhuriwa na wasimamizi wa sheria katika mikoa mbalimbali nchini.

Reticia amesema wapo wanaume wengi wanaofanyiwa unyanyasaji mkubwa na wa kutisha na wake zao lakini kwa madai ya kuficha aibu hiyo wameendelea kutoeleza ukweli.

Amesema miongoni mwa unyanyasaji wanaofanyiwa ni pamoja na kipigo cha mara kwa mara ambacho wamekuwa wakikipata kutoka kwa wake zao na wao kulazimika kudanganya hususani wanapoulizwa juu ya majeraha wanayoyapata.

No comments:

Post a Comment