Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Sunday, June 17, 2012

MOMBA WATAKIWA KUWA NA MSHIKAMANO

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro amewataka viongozi na wananchi wa wilaya Mpya ya Momba kuhakikisha wanakuwa na mshikamano ili kuiwezesha wilaya yao kupata maendeleo kwa haraka.MKUU WA MKOA WA MBEYA ABBAS KANDORO AKIPEWA SILAYA ZA JADI ZA WANYAMWANGA KABILA LA WAKAZI WA WILAYA MPYA YA MOMBA
Kandoro ameyasema hayo katika sherehe za kuipongeza serikali kwa kukubali ombi la kuanzishwa kwa wilaya ya Momba zilizoandaliwa na wananchi na kufanyika katika kijiji cha Chitete  yalipo makao makuu ya wilaya hiyo.
Amesema migongano na vitendo vya uvunjifu wa amani vinaweza kusababisha wilaya yao kuchelewa kuyafikia maendeleo hatua ambayo itakuwa inatofautiana na malengo ya serikali ya kuchukua maamuzi kuanzisha wilaya mpya.

Amewataka maofisa na watendaji wa serikali wilayani hapo kuhakikisha wanazingatia uadirifu katika utendaji kazi wao wakiogopa uonevu lakini pia wakizingatia kutokuwa waoga.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya hiyo Abiud Saidea ameahidi kushirikiana kwa karibu na watendaji pamoja na wananchi huku pia akiiomba serikali ya mkoa kuhakikisha inakuwa karibu na kuipa upendeleo wilaya yake katika mipango mbalimbali ya kimaendeleo iliyopo.

No comments:

Post a Comment