Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Saturday, June 16, 2012

MWENGE WA UHURU WAWASILI ZANZIBAR UKITOKEA MKONI LINDI

Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi
 Mwenge wa Uhuru leo Umeingia Kisiwani Zanzibar
ambapo Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Kapteni Honest Mwanossa
ameweka mawe ya msingi na kuzindua miradi mbali mbali ya maendeleo
katika mkoa wa mjini Magharibi.
Akiweka
jiwe la Msingi la kituo kidogo cha Polisi cha Kombeni Mjini Zanzibar,
kiongozi huyo amewataka viongozi wa Kitaifa kuepuka ufujaji wa fedha za
wananchi na kujiingiza kwenye ufisadi na kuwataka wafanye mambo kwa
maslahi ya Taifa.
Awali
katika risala yao kwa Kiongozi wa mbio za Mwenge, wananchi wa Makombeni
wameliomba Jeshi la Polisi kuangalia uwezekano wa kuharakisha ujenzi wa
kituo hicho ili kupunguza kero ya uhalifu katika eneo hilo.
Moja
ya ujumbe wa Mwenge wa mwaka huu umehimiza umuhimu wa kila mmoja wetu
kuhesabiwa katika Sensa ya kitaifa ili kuiwezesha Serikali kupanga vema
maendeleo kwa wananchi wake.
Mwenge huo umewasili kisiwani Zanzibar ukiotokea mkoa wa Lindi ambako ulikuwa ukikimbizwa katika wilaya mbalimbali za mkoa huo.
Ukiwa
Kisiwani hapa, Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa atazindua na kuweka
mawe ya msingi ya miradi mbalimbali ya maendeleo katika wilaya na mikoa
yote mitano ya Unguja na Pemba kabla ya kuendelea na mbio zake katika
mikoa mingine ya Tanzania Bara.

No comments:

Post a Comment