Ajali
hiyo imetokea leo(Juni 5) majira ya saa 6:30 eneo la mlima Mzalendo Igawilo
nje kidogo ya jiji la Mbeya ambapo Coasta yenye namba T 188 AWE iliyokuwa imejaza abiria ikitokea
jijini kuelekea wilayani Kyela liligongana na Lori lenye namba T 658 ASJ Scania lililokuwa
na tela lenye namba T 150 ASN likitokea Malawi.
Mashuhuda
wa tukio hilo wamesema chanzo cha ajali hiyo ni kufeli kwa breki za Scania
iliyokuwa ikishuka mlima mkali na maarufu kwa ajali kutokana na kuwa na kona
nyingi na ndipo likaivaa coasta na kusababisha majonzo hayo.
Kwa
mujibu wa maafisa wa jeshi la polisi waliozungumzia tukio hilo baada ya
kuteremsha miili ya watu waliokufa katika ajali hiyo na kuiingiza katika chumba
cha kuhifadhia maiti kwenye hospitali ya rufaa Mbeya watu waliokufa ni 10 na 19
walijeruhiwa.
Maofisa
hao wameoomba kutotajwa majina kutokana na kutokuwa wasemaji wa jeshi la polisi
walisema waliokufa eneo la tukio ni tisa na mmoja alifia katika hospitali ya
rufaa wakati akiendelea kupata matibabu pamoja na majeruhi wengine.
Wamesema
kati ya waliokufa wapo wanaume saba akiwemo dereva aliyefahamika kwa jina la
Mwasa Diamond(32) mkazi wa eneo la CCM Ilomba jijini Mbeya huku aliyefia
hospitali akifahamika kwa jina la Titus Mbeye pamoja nao wanawake watatu akiwemo mmoja aliyetajwa kuwa mjamzito lakini wote
hawakufahamika majina wala makazi yao.
Harakati
za kumtafuta kamanda wa polisi mkoani hapa Athuman Diwani zimegonga mwamba
baada kutopatikana ofisini na hata alipopigiwa simu yake ya kiganjani yenye
namba 0787323444 haikupokelewa.
No comments:
Post a Comment