SERIKALI
mkoani Mbeya imeombwa kulijengea uwezo Baraza la watoto walio na Ulemavu ili
liweze kufanya kazi zake za kuwatetea watoto hao kama ilivyotarajiwa wakati wa
kuanzishwa kwake.WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI CHITETE WILAYANI MOMBA MKOANI MBEYA WAKIIMBA KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA KIMKOA
Ombi
hilo limetolewa katika risala ya baraza hilo iliyosomwa na mtoto Daria Njovu
mwanafunzi wa shule ya msingi Mwenge ya wilayani Mbozi kwenye maadhimisho ya
mtoto wa Afrika yaliyofanyika kimkoa katika kijiji cha Chitete wilayani Momba.BAADHI YA WAKAZI WA WILAYA YA MOMBA WALIOFIKA KATIKA MAADHIMISHO YA MTOTO WA AFRIKA
Daria
amesema baraza hilo linakabiliwa na changamoto nyingi hali inayolazimu kuomba
msaada wa serikali na wadau wengine katika kulijengea uwezo ili litimize kazi
zake.
Amezitaja
changamoto zinazoendelea kuwakabili watoto walio na ulemavu kuwa ni pamoja na
ukosefu wa matibabu,elimu duni kwa jamii juu ya walemavu na pia walemavu kusoma
katika shule za mchanganyiko na watoto wa kawaida.
Wameiomba
pia serikali ya mkoa kuanzisha shule za sekondari maalumu kwaajili ya walemavu
ili kuwawezesha watoto wanaohitimu elimu ya msingi na kufaulu waweze kujiunga
na shule hizo na kuendelea na masomo ya elimu ya juu kama ilivyo kwa enzao wasio
na ulemavu.
Kwa
upande wake mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro amesema kuwaweka watoto walio
na walemau katika shule za mchanganyiko na wasio na ulemavu kunalenga kuondoa
dhana ya kuwatenga walemavu.
No comments:
Post a Comment