Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Thursday, June 7, 2012

MWANAFUNZI AJINYONGA

Mwandishi wa Blogu hii ya kijamii ya Lyamba Lya Mfipa kutoka mji mdogo wa Tunduma  Azaria Mwanyika,anaripoti kuwa
 
Mwanaskauti na pia mwanafunzi wa kidato cha nne shule ya sekondari mwalimu J.K.Nyerere iliyopo wilayani Momba katika mji mdogo waTunduma aliyejulikana kwa jina la Boazi Essau Mwalusanya amejinyonga hadi kufa.
 
Sababu za kujinyonga kwake hazijajulikana mpaka sasa. kabla ya kujinyonga mwanafunzi huyo alikuwa akiongea lugha mbalimbali ikiwemo lugha ya Kiarabu na alikaliliwa akisema atakufa mwezi wa sita na kudai kuwa atakumbukwa kama msanii maarufu aliyekufa hivi karibuni kwa mtikisiko wa ubongo. mwanafunzi huyo amezikwa tarehe 6/6/2012 katika makaburi ya migimbani mjini Tunduma.
 
Wakati huo huo kumetokea fujo (timbwili) kubwa katika shule hiyo kwa wanafunzi kuchomana visu, shule hiyo imekuwa ikijihusisha na mikasa mbalimbali hasa ya utovu wa nidhani ikiwemo uvutaji bangi hivyo kuwapa wakati mgumu walimu wao katika shughuli za ufundishaji.

No comments:

Post a Comment