Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Monday, June 11, 2012

RPC APANIA MAJAMBAZI

 KAMANDA mpya wa polisi mkoani Mbeya Athuman Diwani ametoa onyo kali kwa watu wanaojihusisha na matukio mbalimbali ya uharifu ikiwemo ujambazi akisema wakati wao umekwisha hivyo wanapaswa kufanya shughuli nyingine zilizo halali.

Kamanda Diwani ameyasema hayo leo(JUNI 11) alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake ikiwa ni kikao chake cha kwanza kukifanya na wana tasnia hiyo tangu alipohamishiwa mkoani hapa.

Amekiri mkoa wa Mbeya kuwa miongoni mwa mikoa nchini ambayo majina yake hayatajwi vizuri kutokana na kukithiri kwa vitendo vya uharifu hali aliyosema ni changamoto kwake kuandaa mikakati madhubuti itakayourejesha mkoa katika hali ya amani na utulivu.

Amevitaja vitendo vya upigaji nondo kuwa miongoni mwa vile vinavyouchafua mkoa na kuahidi kuwa mikakati ya kuwabana wale wote wanaohusika na vitendo hivyo upo tayari na kinachofuata sasa ni utekelezaji.

Hata hivyo alisema ushirikiano wa dhati baina ya jeshi la polisi na wadau wengine ni jambo muhimu litakalowezesha mikakati yake kufanikiwa huku akisisitiza kuwa wadau kutoa taarifa za uhakika juu ya uwepo wa waharifu ama mipango ya kiharifu ni muhimu pia.

No comments:

Post a Comment