MTU mmoja amefariki dunia mkoani Mbeya baada ya
kuangukiwa na magogo ya Mbao alipojaribu kuruka kutoka katika gari la mizigo
lililokuwa likikaribia kupinduka.
Msemaji wa jeshi la polisi mkoani Mbeya Majaliwa
Mbogella amesema tukio hilo limetokea Juni 7 mwaka huu majira ya saa 2:30
asubuhi katika kijiji cha Lualanje wilayani Chunya likihusisha gari yenye namba
T 732 BWV aina ya Fuso.
Mbogela amemtaja marehemu katika tukio hilo kuwa ni Sani
Mgavi(28) mkazi wa Mufindi mkoani Iringa aliyekuwa mkulima na pia fundi wa
kupasua mbao .
Amesema Mgavi amekutwa na mauti baada ya kuangukiwa
na magogo ya mbao yaliyokuwa yakisafirishwa na gari aliyokuwa amepanda lakini
walipofika katika kijiji cha Lualanje gari hiyo ilikwama kwenye mchanga na kulalia
upande.
Kufuatia hali hiyo,fundi huyo aliyehisi gari
inapinduka aliamua kuruka na kwakuwa alirukia upande lilikolaria gari magogo
yalimporomokea na kukatisha uhai wake papo hapo.
No comments:
Post a Comment