Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Saturday, June 16, 2012

TWIGA STARS AIBU TUPU

Timu ya taifa ya wanawake ya Ethiopia imeifunga Twiga Stars ya Tanzania goli 1-0 katika mchezo wa marudiano kutafuta tiketi ya kucheza Fainali za Nane za Afrika kwa Wanawake (AWC) zitakazofanyika Novemba mwaka huu nchini Equatorial Guinea uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni leo.
  
Katika matokeo ya mechi ya awali  Twiga Stars ilifungwa mabao 2-1 na na sasa timu ya Ethiopia imefuzu kucheza fainali hizo za Equatorial Guinea.  Nchi ambazo tayari zimefuzu kwa fainali hizo ni wenyeji Equatorial Guinea na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).
 KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA YA WANAWAKE YA ETHIOPIA

No comments:

Post a Comment