Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Thursday, June 7, 2012

MCHUNGAJI TAG APORWA MILIONI 4


WATU watatu wasiofahamika majina wala makazi wamemteka mchungaji wa kanisa la Asemblies Of God (TAG)  la Iyunga jijini Mbeya na kumpora fedha taslimu za kanisa kiasi cha shilingi milioni 4 laki 9 na 3000.

Msemaji wa jeshi la polisi mkoani Mbeya Majaliwa Mbogela amemtaja mchungaji huyo kuwa ni Husein Enock(40) mkazi wa Iyunga na kuwa amekutwa na mkasa huo Juni 5 mwaka huu majira ya saa 8:00 za mchana alipotoka kuchukua fedha hizo katika tawi la benki ya Biashara ya Afrika (CBA) lililopo mwanjelwa jijini hapa.

Mbogela amesema baada ya mchungaji Enock kutoka nje ya benki hiyo alikuta gari aina ya Noah  yenye namba asiyoifahamu na ndani yake kulikuwa na watu watatu aliokuwa akiwafahamu kwa sura na ndipo wakampa msaada wa rifti kwenda kanisani kwake Iyunga.

Tofauti na matarajio ya mchungaji huyo,dereva wa gari hiyo baada ya kuingia barabara kuu alielekea mwelekeo tofauti wa kwenda mkoani Iringa na walipofika katika eneo la Mlima Nyoka nje kidogo ya jiji la Mbeya walimnyang’anya fedha zote na kumtelekeza hapo kisha wao wakatoweka.

No comments:

Post a Comment