Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Tuesday, June 19, 2012

NAANZA NA WANAOJICHUKULIA SHERIA MIKONONI

MKUU wa wilaya ya Rungwe Chrispin Meela ameonya vitendo vya uharibifu wa mali vinavyofanwa na baadhi ya wananchi wanaojichukulia sheria mikononi kwa kisingizio cha kuwa na hasira akisema vinapaswa ukoma mara moja.
 
Akizungumza na LYAMBA LYA MFIPA,Meela amesema hayuko tayari kuona uharibifu wa aina hiyo ukiendelea kutokea wialayani kwake na atahaikisha hatua za isheria zinachukuliwa dhidi ya wananchi yeyote atakayebinika.
 
Ametolea mfano vurugu za hivi kribuni za wanafunzi katika seminari ya Minow zilizosababisha hasara ya zaidi ya ilioni 50 kutokana na mali mbalimbali zilizoharibiwa pamoja na zile za Kiwira mbapo wananchi walivunja milango ya ofisi a kijiji na Zahanati kushinikiza kujiuzulu kwa mwenyekiti wa kijiji chao.
 
Amesema uharibifu wa mali kiasi hicho haulengi kujenga bali kubomoa maendeleo yanayopiganiwa kila siku kuyafikia hivyo ni vema wanaosababisha hali hiyo wakadhibitiwa ka uchukuliwa sheria kali ili iwe mfano kwa wengine.
 
Amelitupia lawama jeshi la polisi wilayani hapo akisema linachangia kwa kiasi kikubwa kufanyika ka vitendo hivyo na kuwataka maafisa wa eshi hilo kubadilika iutendaji iwao wanataka kuendana na kasi ya uongozi wake.
 
Mkuu huyo wa wilaya ambaye ndiyo kwanza ananza kuitumia nafasi hiyo tangu alipoteuliwa aliwataka wadau mbaimbali ungana katika ukomesha vitendo vya vunjifu wa amani vinavyoweza kusababisha kuwapotezea muda wa fanya shughuli za kimaendeleo.
 
Ameonya pia wakazi wa wilaya hiyo kutenganisha siasa na utendajikazi iwapo wanalengo la kuiwezesha wilaya yao upiga hatua kimaendeleo.

No comments:

Post a Comment