Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Tuesday, June 5, 2012

BENKI YA POSTA MBEYA YASAIDIA KITUO CHA MPANGO WA DAMU SALAMA KANDA

 WAKIANGALIA UJUMBE WA KILA ANAYECHANGIA DAMU NI SHUJAA ULIOANDIKA KWEENYE TISHETI HIZO
 HAPA MAOFISA HAO WAKIFURAHIA KWA PAMOJA MSAADA ULIOTOLEWA
 MENEJA WA BENKI YA POSTA BWANA JULIUSA AKIFAFANUA JAMBO JUU YA HUDUMA ZINAZOTOLEWA NA BENKI HIYO BAADA YA KUKABIDHI MSAADA
 XXXXXXXXXXXXXXXX HABARI KAMILI XXXXXXXXXXXX
BENKI ya posta nchini tawi la Mbeya leo(Juni5) imekabidhi msaada wa tisheti 150 wenye thamani ya shilingi milioni mbili kwa kituo cha Mpango wa Taifa wa Damu salama kanda ya Nyanda za juu kusini.

Kutolewa kwa msaada wa tisheti hizo zilizo na nembo ya kaulimbiu ya maadhi misho ya damu salama mwaka huu ya KILA MCHANGIAJI DAMU NI SHUJAA kumelenga kusaidia hamasa kwa wadau kuchangia damu.

Akikabidhi msaada huo,meneja wa benki ya Posta tawi la Mbeya Hamphrey Julius amesema kutoa msaada huo kunatokana na benki kutambua kuwa ni taasisi ya umma inayopaswa kurejesha faida kidogo inayopata kwa wananchi ambao ndiyo wamiliki kupitia uchangiaji huduma za kijamii.

Naye Afisa utumishi wa kituo hicho cha damu salama Kundael Saria amesema msaada huo umewafikia kwa wakati na kuwaomba wadau wengine kuiga mfano huo ili kuwezesha hamasa ya uchangiaji damu.

Saria amesema kituo hicho kinategemea nguvu ya wadau mbalimbali katika kuendelea kutoa hamasa ya uchagiaji damu kwa hiari hasa kutokana na ufinyu wa bajeti yake katika kila mwaka wa fedha

No comments:

Post a Comment