KUENEZWA
kwa dhana kuwa Serikali haitambui uchawi kumeelezwa kusababishia matukio mengi
ya wananchi kujichukulia sheri amikononi ya kuwaua watu wanaohisiwa kuwa
wachawi pamoja na kuharibu mali zao.
Mmoja
wa maofisa wa kituo cha Sheria na Haki za binadamu (LHRC) Leticia Petro ameyasema
hayo na kubainisha kuwa katika kipindi cha mwaka jana zaidi ya mauaji 600
yametokea nchini yakihusisha wananchi kujichukulia sheria mikononi kwa
kuwatuhumu wenzao uchawi na kuitaja mikoa ya Shinyanga na Mwanza kuwa inaongoza.
Amesema
ni dhana potofu kueleza kuwa serikali haiamini uwepo wa uchawi ilikhali tangu
mwaka 1928 iliundwa sheria ya Uchawi nchini na mwaka 2002 ikafanyiwa
marekebisho.
Kwa
upande wao washiriki wa semina ya mafunzo ya Wasaidizi wa sheria iliyofanyika
jijini Mbeya walilalamikia baadhi ya viongozi wa serikali na jeshi la polisi katika
ngazi za wilaya wakisema wamekuwa wakiwadanganya wananchi kuwa serikali
haiamini uchawi badala ya kuwaelimisha taratibu zinazopaswa kufuatwa pale
wanapomtuhumu mtu kuwa mchawi.
No comments:
Post a Comment