HALMASHAURI
ya wilaya ya Mbarali imewahakikishia wakazi wilayani hapa kuwa siku chache zijazo
huduma za afya zitapanuliwa kwa zahanati
saba na kituo kimoja cha afya kufunguliwa.
Kaimu
mkurugenzi wa halmashauri Aswege Kaminyoge ametoa uhakika huo alipotembelea
na kukagua zahanati hizo na kusema kabla ya kumalizika kwa mwezi juni
zitakuwa zimeanza kutoa huduma.
Kaminyoge
amesema kufunguliwa kwa zahanati na kituo kimoja cha afya licha ya kusaidia
wagonjwa wengine,kutanusuru afya za akina mama wajawazito ambao kwa sasa
wanakabiliwa na adha ya kujifungulia majumbani mwao.
Kwa
upande wake Mganga mkuu wa wilaya hiyo,Dkt.
Boniface Kasululu
amekiri kuanza kufanya kazi kwa zahanati saba na
kituo kimoja cha afya kutapunguza kwa kiasi kikubwa vifo vya akinamama wajawazito
na watoto
vilivyokuwa vikitokana na kutopatikana kwa huduma za wataalamu mara
wanapojifungulia majumbani ama njiani wanapotembea umbali mrefu kuja hospitali
ya wilaya.
Wakizungumzia
adha waliyokuwa wakiipata wakazi wa Kijiji cha Mlungu Jamila Kalinde na Wilison
Mbedule walisema wakazi wa kijiji hicho na vingine vya jirani wamekuwa wakitembea
umbali wa zaidi ya kilometa 40 kufuata huduma ya afya katika Kituo cha afya cha
Kwatwanga, kilichopo katika mkoni Iringa.
No comments:
Post a Comment