WANAFUNZI
24 wa shule ya sekondari ya seminari ya Manow ya wilayani Rungwe mkoani Mbeya
leo(Juni 15) walifikishwa mahakamani kusomewa shitaka la kufanya vurugu
zilizopelekea uharibifu mkubwa wa mali za shule zenye thamani ya zaidi ya
shilingi 50 milioni.
Mwenyekiti
wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya mkuu wa wilaya Chrispin Meela
amethibitisha wanafunzi hao kufikishwa mahakamani alipozungumza na RFAjijini Mbeya ikiwa ni siku moja tangu tukio hilo litokee.
Meela
amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia juni 14 baada ya uongozi wa shule
kuwataarifu wanafunzi kuwa kwa usiku huo watalazimika kula chakula kingine
badala ya wali kutokana na mchele uliokuwepo kuisha huku mwingine ukiwa
haujafikishwa shuleni hapo.
Amesema
baada ya kuambiwa hayo wanafunzi hao waliwaongoza wenzao kufanya vurugu kwa
kuharibu mali mbalimbali ikiwemo kuvunja milango na madirisha ya majengo
mablimbali yakiwamo madarasa.
Mkuu
huyo wa wilaya tayari amekwisha ifunga shule hiyo hiyo hadi tarehe Julai 7
mwaka huu wanafunzi watakaporudi tena na kuwataka wale wa kidato cha pili,
tatu, Nne na sita kwa kuwa imeonekana kuwa ndio viongozi wa uharibifu huo wajapo
shuleni hapo waje na wazazi wao na maelezo binafsi kwa barua.
No comments:
Post a Comment