Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Saturday, June 16, 2012

WAANDISHI WA HABARI WANAOTUHUMIWA KUPOKEA RUSHWA WAFIKISHWA MAHAKAMANI JIJINI ARUSHA

 HALI ILIVYOKUWA MAHAKAMANI HAPO WAKATI WA KESI YA WAANDISHI HAO
MMOJA WA WATUHUMIWA HAO AKIWASILI MAHAKAMANI
Na Idd Uwesu- Arusha yetu
Wafanyakazi watatu wa kampuni ya new habari cooparation waliokamatwa na askari wa kikosi cha kuzuia na kupamaba na rushwa nchini takukuru kwa madai ya kuomba na  kupokea rushwa ya shilingi laki mbili kati ya milioni moja na laki nane wamefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa arusha kujibu tuhuma zinazowakabili

Watuhumiwa hao wamesomewa mashataka yao mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya mkoa wa arusha,Yohana Myombo,na mwendesha mashitaka wa taasisi ya kuzuia na kupamabana na rushwa  Hamidu Simbano amedai kuwa  watuhumiwa hao wanakabiliwa na mashitaka mawili ikiwemo kushawishi na kudai rushwa.

Katika eneo la mahakama ya hakimu mkazi mkoa arusha watuhumiwa hao waliwasili,huku kando waandishi wa habari pamoja na ndugu jamaa wakiwa wamefika katika eneo hilo kwa shauku ya kufahamu nini kitajiri katika kesi hiyo.

Mwendesha mashitaka wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU mkoa wa arusha,Hamidu Simbano ameiambia mahakama kuwa watuhumiwa hao watatu wanadaiwa kumshawishi mtumishi wa Shirika la Umeme TANESCO wilaya ya Monduli kutoa rushwa kwa madai ya kutokidhi vigezo vya ajira yake.

Washitakiwa hao watatu wote wanashitakiwa kwa kosa moja la kushawishi na kudai rushwa ya shilingi milioni 1.5, ambapo mshitakiwa wa tatu, Mwita Chomete yeye anadaiwa kuwa mnamo majira ya saa 10 jioni katika wilaya ya Monduli alipokea shilingi laki mbili kwa niaba ya Masyaga Matinyi.

Washitakiwa wote walikana mashitaka hayo na wako nje kwa dhamana ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi juni 29 mwaka huu.
 
HABARI NA PICHA NI KWA HISANI YA MTANDAO WA www.arushayetu.blogspot.com

No comments:

Post a Comment