Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Thursday, June 7, 2012

UMISSETA MBEYA WAENDA RUKWA

TIMU ya mkoa wa Mbeya kwa mashindano ya shule za sekondari(Umisseta) alhamisi hii imeondoka kuelekea mkoani Rukwa tayari kwa kushiriki ngazi ya kanda ya ndanya za juu kusini ya michuano hiyo itakayoanza Ijumaa ya wiki hii.

Timu hiyo imeondoka ikiwa na jumla ya wachezaji 140 wa michezo mbalimbali na kati yao wakiwemo Wasichana 71 na wavulana 69 waliopatikana kupitia mashindano hayo ngazi ya mkoa.

Meneja wa timu hiyo George Mbijima ambaye pia ni afisa michezo,vijana na utamaduni mkoa wa Mbeya amesema pamoja naye timu imeongozana na viongozi wengine 11 wakiwamo walimu wa michezo husika,Mwenyekiti wa timu Juma Kaponda, na mratibu Kasekenya Michael.

Mbijima amewahakikishia wakazi wa mkoa wa Mbeya kuwa upo uwezekano mkubwa wa timu hiyo kurejesha historia ya ushindi wa mwaka jana kutokana na maandalizi mazuri iliyofanya wakati ikiwa kambini kujiandaa.

No comments:

Post a Comment