HATIMAYE matumaini ya mradi mkubwa wa
ujenzi wa miundombinu ya maji ya bomba katika kata ya Itagano Jijini Mbeya unaofadhiriwa
na Benki ya Dunia (WB) kwa mkopo yameanza
kuonesha dalili baada ya halmashauri ya jiji kuukabidhi kwa mkandarasi kwa
ajili ya kuanza kutekelezwa.
Meya wa jiji la Mbeya Athanas Kapunga
leo (Juni 11) ameiwakilisha halmashauri wakati wa kutiliana saini ya mkataba
wa utekelezaji wa ujenzi wa mradi huo na kampuni ya Geotech ya Jijini Mbeya.
Kwa mujibu wa kaimu mkurugenzi wa Jiji la
Mbeya, Seko Nkusa,mradi huo utajengwa kwa gharama ya shilingi milioni
293,553,571.21 na utekelezaji wake
unaanza mara moja baada ya kusainiwa kwa mkataba na ni wa muda wa miezi sita.
Nkusa amesema ujenzi wa mradi huo
utasimamiwa na mhandisi mshauri, kampuni ya COWI ya Jijini Dar es Salaam kwa
gharama ya shilingi milioni 29.196.
Kwa upande wake meya Kapunga ameishukuru
Serikali kwa kusaidia upatikanaji wa mfadhili huyo aliyekubali kutoa fedha za
ujenzi wa mradi huo huku akisema hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya
uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2010.
Naye
diwani wa Kata hiyo Abel Mbwiga Ndalama amesema kuwa ujio wa mradi huo
ni ukombozi kwa wananchi wa kata yake ambao hivi sasa wanatumia maji ya visima
vyenye maji ambayo siyo safi wala salama.
No comments:
Post a Comment