Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Friday, June 15, 2012

SAFARI YA DOGO JANJA KURUDI KWAO

Dogo Janja akiwaaga washikaji.
Dogo Janja akiagana na kaka yake mwenye t-shirt ya bluu yenye mistari.
Akiingia ndani ya basi.
Akiwa ndani ya basi.
Safari ya kuelekea AR.
Tiketi ya Dogo Janja.

Jana kwenye AMPLIFAYA ya CLOUDS FM Msanii Madee wa Tip Top Connection ambae ndio alikabidhiwa na wazazi kumlea na kumsimamia Dogo Janja aliamplfy kuhusu sababu za kumrudisha Dogo Janja mikononi mwa wazazi wake baada ya kudai kumshindwa.
Madee kasema “Dogo Janja aliyekuwa Form II, Makongo High School kakataa kusoma kwa hiyo mimi siwezi kukaa nae wakati hataki kusoma, nilikuwa safarini Iringa na Mbeya ambapo baada ya kurudi mwalimu wake wa darasa alinipigia simu na kunipa pole kwa sababu Dogo Janja anaumwa, nikashtuka ikabidi nimpigie nikawa simpati kwenye simu, nikaenda nyumbani kwa Tunda Man alipokuwepo na alipojua nimekuja akajificha alikuwa anataka kunikimbia nikampiga sana vibao, kweli nilimpiga ambapo kesho yake baada ya kuamka nikamuuliza unataka kusoma au kuzurura mtaani? akajibu kwamba anataka kwenda kusoma Arusha ikabidi nimpigie baba yake palepale ambapo mzee wake alniomba nisimrudishe Arusha niendelee kukaa nae”
Madee ameendelea kusema kwamba “nilimwacha nyumbani baada ya kuchukua simu yake ambapo nilikuta vitu vingi sana vya kishenzi shenzi kaviandika na ninavyo mpaka leo kwa ajili ya ushahidi, vimeniumiza hasa kwa mtu kama mimi ambae najua nimemtoa wapi, kaandika kuhusu uchafu mbaya na kingine kinanihusu mimi ambacho hapaswi kusema kwa mtu kama yeye, baada ya hapo msimamo wake ulikuwa vilevile kwamba anataka kurudi kwenda kusoma Arusha, jioni tukakaa kikao (juzi) na kaka yake na watu wengine na mimi nikampa baraka zote”
Kwenye sentensi nyingine Madee amesema “kwa wiki iliyopita na wiki hii Dogo Janja alitoroka kwenda shule kwa siku tatu na hii ni mara ya pili ambapo mara ya kwanza nilimpeleka shule na kumchapa mbele ya wanafunzi wenzake, yaani nilivyompeleka shule wanafunzi wenzake mpaka walikuwa wanamshangaa, alisingizia vitu vingi vya uongo alikuwa ananidanganya mimi nyumbani na siku hiyo ndio nilimkuta Ubungo Plaza alikuwa anaogelea na rafiki yake, walimu wake waliniambia hawajamuona shule kwa muda wa wiki moja”
PICHA NA HABARI KWA HISANI YA MILLARDAYO.COM

No comments:

Post a Comment