Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Friday, February 3, 2012

MASHABIKI WATAKIWA KUJITOKEZA UWANJA WA SOKOINE JUMAMOSI HII

MASHABIKI wa soka mkoani Mbeya wamepewa wito kujitokeza kwa wingi kushuhudia mchezo wa fungua dimba wa mzunguko wa ligi daraja wa kwanza ambao jumamosi hii utazikutanisha Tanzania Prisons na Mbeya City zote za jijini hapa.

Makamu mwenyekiti wa chama cha soka mkoani hapa Ben Mwamwaja ametoa wito huo na kusema maandalizi ya mchezo huo utakaopigwa kwenye uwanja wa Sokoine yamekamilika.

Timu ya Tanzania Prisons itashuka uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kufungwa goli 1-0 na Mbeya City kwenye mchezo uliochezwa katika mzunguko wa kwanza.

Akizungumzia mchezo huo kocha wa Mbeya City Juma Mwambusi amewataka mashabiki wa timu yake kufika kwa wingi uwanjani ili waweze kujionea maboresho yaliyofanyika ndani ya kikosi hicho.

Katika mzunguko wa kwanza uliomalizika mwishoni mwa mwaka jana Mbeya City iliumaliza ikiwa na jumla ya pointi 13 huku Tanzania Prison wakiwa na pointi tano.

No comments:

Post a Comment