Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Wednesday, February 8, 2012

PRISONS YAICHAPA SMALL KIDS 2-1

Mchezo wa ligi soka daraja la kwanza kati ya Tanzania Prisons ya Mbeya na Small Kidd iliyokuwa ya Rukwa umemalizika kwa Tanzania Prisons kuibuka mshindi kwa goli 2-1.

Goli la kwanza limepatikana dakika ya 6 kupitia kwa mchezaji Peter Michael na dakika ya 29 likafungwa na mchezaji huyo kwa penati huku Small Kids wakipata goli lao dakika ya 12 kupitia mchezaji Abubakari Makida.

Nako Songea Mbeya City imetoka sare ya 1-1 na JKT mlale wakati Iringa Majimaji ya songea wamekubali kipigo  cha goli 1-0 toka kwa Polisi ya Iringa

No comments:

Post a Comment