Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Monday, February 6, 2012

MOTO WATEKETEZA BWENI LA WAANAFUNZI


BWENI moja la wanafunzi wa kike katika shule ya sekondari ya Swila iliyopo mbalizi wilayani Mbeya limeteketea kwa moto.

Tukio hilo limetokea Februari 5 mwaka huu majira ya saa tano asubuhi  wakati wanafunzi wachache wakiendelea na shughuli za usafi shuleni hapo huku wenzao wakiwa wamekwenda kushiriki ibada ya jumapili.

Kamanda wa polisi mkoani hapa Sdvocate Nyombi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema pamoja na mali nyingine moto huo umeteketeza vitannda 40 vya wanafunzi lakini thamani ya malizo zote haijafahamika bado.

Kamanda Nyombi ametaja chanzo cha moto huo kuwa ni hitlafu ya umeme iliyotokea shuleni hapo na kwamba hakuna madhara yaliyotokea kwa binadamu na uchunguzi zaidi unaendelea kuhusiana na tukio hilo.

No comments:

Post a Comment