Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Monday, February 6, 2012

MAUAJI YATOKANAYO NA TUHUMA ZA UCHAWI YAENDELEA KUTIKISA MBOZI

Mkazi wa Kijiji cha Saanane  Wilayani Mbozi mkoani hapa,Nicodemu Saanane(50) mkulima ameuawa kwa kukatwa kwa na kitu chenye ncha kali  katika sehemu za tumboni,na watu wasiofahamika.
 Nyombi amesema kuwa tukio hilo lilitokea febuari 4 mwaka huu majira 4.30 katika kijiji cha Kisanu Wilayani Mbozi mkoani Mbeya.

Amesema kuwa marehemu alitoweka  nyumbani kwake tangu febuari 3 mwaka huu majira ya saa 5 asubuhi katika mazingira ya kutatanisha na kuelekea kusikojilikana .

Amesema kuwa chanzo cha mauji hayo ni imani za kishirikina kwani marehemu alikuwa anatuhumiwa na  wanakijiji wenzake kuwa mchawi kijijini hapo,na kwamba msako mkali unaendelea kuwabaini watuhumiwa waliuohusika.

No comments:

Post a Comment