Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Thursday, February 9, 2012

MGOMO WA MADAKTARI-SERIKALI YASIMAMISHA KAZI UONGOZI

Serikali imemuandikia Barua ya kumsimamisha kazi Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bi.BLANDINA NYONI na Mganga Mkuu wa Serikali Dokta DEO MTASIWA ili kupisha uchunguzi dhidi ya malalamiko ya Madaktari.
                                     Hata hivyo suala la Waziri wa Afya na Naibu Wake limeachwa kwa Rais JAKAYA KIKWETE kwa kuwa ndiye mwenye dhamana na Viongozi hao.

 Taarifa hiyo imetolewa leo na Waziri Mkuu Mheshimiwa MIZENGO PINDA wakati akizungumza na Makundi kadhaa ya Madaktari katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya jitihada za kumaliza mgomo wa Madaktari.
 
Pinda amesema vyombo vya dola kwa sasa vinafanya kazi ya uchunguzi ili kubaini ukweli wa malalamiko hayo wakati watumishi hao wakiwa nje ya ofisi na kwamba atateuliwa Kaimu Mganga Mkuu na Kaimu Katibu Mkuu kuanzia sasa ili kushika nafasi hizo.
Wakati hayo yakiendelea,mjini Dodoma bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepokea taarifa ya Kamati yake ya Huduma za Jamii ambayo ina mapendekezo kadhaa kuhusu hatua za kuchukua ili kumaliza mgogoro unaoendelea kati ya Madaktari na Serikali.

No comments:

Post a Comment