Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Sunday, February 5, 2012

SHAMSA VUAI NAHODHA ATAKA WAZEE CCM WAWAPE NAFASI VIJANA

CHAMA cha Mapinduzi CCM kimeaswa kutopuuza vijana iwapo kina nia ya dhati ya kwenda na wakati katika mfumo wa vyama vingi uliopo nchini.
Waziri wa Mambo ya Ndani Shamsa Vuai Nahodha ameyasema hayo leokatika maadhimisho ya miaka 35 ya chama hicho yaliyofanyika kimkoa katika uwanja wa Kibonde Nyasi Uyole jijini Mbeya.
Nahodha amesisitiza kuwa hivi sasa chama hicho kinahitaji zaidi nguvu ya vijana ili kuhimili ushindani hivyo ili kukinusuru lazima wanaCCM wakafanya maamuzi ya kuwapa nafasi vijana katika uchaguzi unaofanyika mwaka huu.
Amesema maneno yake hayamaanishi kuwadharau wazee bali ni kutokana na kutambua kuwa mfumo wa vyama vingi si lelemama bali unahitaji watu walio na nguvu ya kujibu mapigo papo kwa papo na si nguvu ya wazee wanaotafutiza maneno ndipo wajibu.
Amewasihi wazee ndani ya chama hicho kutolewa madaraka na kuona kama bado wana faa hali aliyosema ni sawa na kukichimbia chama chao kaburi.

No comments:

Post a Comment