Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Thursday, February 9, 2012

MTOTOA AUAWA KWA KIPIGO AKITUHUMIWA KUIBA

Mtoto aliyetendewa unyama huo amefahamika kwa jina la Pumba Soimbi(6) ambapo amepigwa hadi kufa na shangazi yake Holo China(21) mkazi katika kijiji cha Madibira wilayani Mbarali.

Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Barakanael Masaki amesema tukio hilo limetokea Februari 8 mwaka huu majira ya saa 8:00 mchana nyumbani kwa mtuhumiwa.

Masaki amesema shangazi huyo alimtuhumu mtoto Pumba kuwa alimuibia shilingi 1000 na ndipo alipochukua maamuzi ya kumuadhibu mtoto huyo kwa kumpiga viboko sehemu mbalimbali za mwili na kujemjeruhi vibaya na hatimaye kumsababishia kifo.

Amesema baada ya polisi kumhoji shangazi wa mtoto ambaye anashikiliwa na jeshi hilo amekiri na kusema licha ya wizi wa fedha hizo pia mtoto huyo alikuwa na kiburi akisema kabla ya kumpiga alimtaka ambebe mtoto aliyekuwa analia lakini akakataa.

No comments:

Post a Comment